YouVersion Logo
Search Icon

Yohana 12:37, 38, 39, 40, 41, 42, 43, 44, 45, 46, 47, 48, 49, 50

Yohana 12:37 NEN

Hata baada ya Yesu kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini.

Yohana 12:38 NEN

Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?”

Yohana 12:39 NEN

Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine

Yohana 12:40 NEN

“Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.”

Yohana 12:41 NEN

Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake.

Yohana 12:42 NEN

Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.

Yohana 12:43 NEN

Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.

Yohana 12:44 NEN

Yesu akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma.

Yohana 12:45 NEN

Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma.

Yohana 12:46 NEN

Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.

Yohana 12:47 NEN

“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.

Yohana 12:48 NEN

Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.

Yohana 12:49 NEN

Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema.

Yohana 12:50 NEN

Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”