YouVersion Logo
Search Icon

Yohana 12:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11

Yohana 12:1 NEN

Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi.

Yohana 12:2 NEN

Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu.

Yohana 12:3 NEN

Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

Yohana 12:4 NEN

Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema

Yohana 12:5 NEN

“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300 na fedha hizo wakapewa maskini?”

Yohana 12:6 NEN

Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

Yohana 12:7 NEN

Yesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu.

Yohana 12:8 NEN

Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”

Yohana 12:9 NEN

Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Yesu alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Yesu, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua.

Yohana 12:10 NEN

Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia

Yohana 12:11 NEN

kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini.